Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja leo Machi 07, 2025 amezindua kamati ya MTAKUWWA Wilaya ya Chamwino ambayo ni Mpa go Wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya wanawake na watoto.
Uzinduzi umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati hiyo.
Akijibu hoja ya mjumbe aliyetaka kufahamu majukumu ya kila mmoja wao Mhe. Mayanja amesema muongozo umeanisha majukumu ya jumla ya kila mjumbe anayopaswa kutekeleza. Aliendelea kusema kuwa kila mjumbe anakundi anàlofanya nalo kazi.
Alitolea mfano unamkuta mtito anapigwa isivyo kawaida, hutakiwa kupita na kuacha hivyo bali unatakiwa kutoa elimu na kutoa taarifa juu ya ukatili huo.
Vile vile alitoa mfano kuwa Afisa lishe anakutana na mtoto mwenye utapiamlo, huo pia ni ukatili anapaswa kuchukua hatua ili mtoto apate matibabu, hali kadhalika kwa Afisa Ustawi umekutana na mtoto ambaye ametelekezwa na wazazi wake anapaswa amchukue amtafutie makazi.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewashukuru Taasis ya KATUKA Paralegal Organization kupitia mradi wao wa SAUTI YA MWANAMKE, mradi wa kuongeza upatikanaji wa hakikwa wanawake, wasichana na makundi maalum kwa kuwezesha kamati hiyo kuzinduliwa kupitia ufadhili wao.
Mradi wao huo unatekelezwa katika kata tatu za Membe, Makang'wa na Chilonwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.