Kaimu Afisa elimu idara ya elimu msingi Mwl Agripina Kanyabuhura amewaongoza mamia ya wananchi wa kijiji cha Mguba kujitolea nguvu kazi kwenye ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Majengo mapya kijiji cha Mguba kata ya Ikombolinga wakati wa mkutano wa kijiji hicho uliofanyika septemba 06, 2021.
Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuhamasisha wananchi wa kijiji hicho kujitolea nguvu kazi katika maendeleo ya Kijiji cha Mguba Mwl Kanyabuhura amewaasa wananchi hao kujitoa kwa moyo na kuchangamkia fursa za maendeleo zinazoletwa kwenye kijiji chao.
Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kata na Kijiji akiwemo Diwani wa kata ya Ikombolinga Mhe. Mtemi Matonya umefanyika ilikuhamasisha wananchi hao kushirikiana na viongozi wao katika kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya elimu.
Shule ya msingi Majengo Mapya iliyopo Kijiji cha Mguba ni miongoni mwa shule nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino zilizobahatika kupata fedha za ujenzi wa matundu 12 ya vyoo yenye thamani ya shilingi Milioni 13.
Kaimu Afisa elimu Mwl Kanyabuhura katika ziara hiyo ameambatana na mlezi wa tarafa ya Makang'wa ambaye ni Afisa michezo na utamaduni mwl Nicholaus Achimpota pamoja na Afisa Mipango Bi. Neema Mirumbe.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.