Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemami Jafo (Mb), amewataka watumishi wa wa kada ya Ualimu na watumishi wengine wa Umma kujiunga na Benki ya Biashara ya Walimu ijulikanayo kama “Mwalimu Commercial Bank’ ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na benki hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya kadi za Viza, Mwalimu mobile na Mwalimu Wakala, Mhe Jafo amesema umefika muda kwa maafisa masoko wa benki hiyo kuwatembelea watumishi walimu na wasio walimu kwa ajili ya kuwashawishi waweze kujiunga na benki ya Mwalimu.
Amesema walimu wengi wakijiunga na huduma za benki hiyo kutaiwezesha kukua zaidi, kwani kundi hilo linakadiriwa kuwa na watumishi laki tatu ambao ni asilimia 72.6 ya watumishi wote wa Umma.
‘Kutokana na wingi wenu huu lazima muone ipo haja sasa ya kujiunga kwa wingi, lakini msiishie hapo tu, bali pia wafikieni watumishi wengine wa kada zingine, nalisema hili kwani najua nguvu ya walimu nikubwa na hakuna lakuwashinda’ amesema Jafo
Waziri Jafo amekumbusha kuwa malengo ya kuanzishwa kwa benki hiyo yalikuwa ni kuwahudumia walimu kama wateja wao wakuu lakini kufikia sasa idadi ya walimu waliojiunga kupata huduma za kibenki ni 41,000 tu.
‘Hapa maafisa masoko mnakazi kubwa yakujenga uelewa wa pamoja ili watu wafahamu kwa mba hiki ni chombo chao’ amesema
Akizungumza kuhusu huduma mpya zilizoanzishwa na benki hiyo, Waziri Jafo amesema kuanzishwa kwa huduma hizo ni ishara kuwa huduma zitolewazo na benki hiyo zimeongezeka, hivyo ni jukumu la uongozi wa benki hiyo kuongeza hamasa na ushawishi kwa walimu na watumishi wengine wa umma kujiunga ili kufaidi huduma za benki hiyo.
Uanzishwaji wa huduma hizi, ni ishara kwamba mmeongeza wigo, hata mtu ambaye alikuwa ansita kujiunga na benki yenu, sasa mmepata suluhisho kwani kupitia huduma kama ya Mwalimu Mobile mtu ataweza kufanya muamala eneo lolote.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.