Miongoni mwa agenda za Dunia ni pamoja na utunzaji wa Mazingira na Kila mmoja anao wajibu wa kuhakikisha hali endelevu ya kuhakikisha mazingira yanatunzwa ipasavyo, katika kuunga juhudi hizo Wizara ya nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamezindua mradi wa usambazaji mitungi ya Gesi Kwa Bei ya ruzuku Ili kuwafikia Wananchi wengi zaidi hususani katika Kona zote za Nchi ikiwemo Mkoa wa Dodoma.
Uzinduzi huo umefanyika leo Januari 8, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika viwanja vya Ofisi ya Kijiji Cha Chamwino Ikulu, Halmashauri ya Wilaya Chamwino.
Akizungumza na Wananchi walioshiriki hafla hiyo RC Senyamule amesema" ni Maono ya Mhe. Rais kugawa mitungi 16,530 Kwa wilaya 6 za Mkoa wa Dodoma Kwa bei ya ruzuku, haya ni malengo endelevu ya kidunia ya kuhakikisha nishati safi inapatikana Kwa bei nafuu na Kwa urahisi, thamani tuliyopewa na Rais ni kubwa sana.
"Nitoe rai Kwenu Wananchi, nyie mmepewa mitungi hii Kwa bei pungufu ya Sh.20,800 kwaiyo niwaombe mchangamkie fursa hiyo, lakini pia tumieni Gesi hizo kulingana na maelekezo mliyopatiwa hapa na wataalam", amesema Senyamule.
Aidha RC Senyamule amewataka Wananchi kuwa makini na watu wasiowaaminifu na wasiona nia njema ambao watatumia fursa hiyo Kuwatapeli kupitia vitambulisho vyao vya taifa na kujiingizia fedha kinyume na taratibu.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja ametoa rai Kwa Wananchi kuchangamkia fursa ya ruzuku ya majiko hayo na kuahidi kuwa Wilaya hiyo watakuwa mabalozi wazuri wa Nishati safi ambapo kuyatimiza hayo wameanzisha kampeni ya "nitunze nikutunze" ambayo inahamasisha Kila kaya kupanda miti kuanzia mitano nakuendelea.
Naye kaimu Meneja REA Bw. Emmanuel yessaya amesema mradi huo unagharimu zaidi ya million 813 na mitungi hiyo ya kampuni ya 'lake gas' inauzwa Kwa Bei pungufu ya 50% ambapo mtungi Wenye Gesi utauzwa Kwa Sh. 20,800 pekee na zaidi ya mitungi laki nne itasambazwa nchi nzima.
Hayo yamejiri ikiwa utekelezaji wa adhma ya Rais wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwa ifikapo 2030 zaidi ya 80% ya watanzania kutumia nishati safi na kuepukana na Matumizi ya nishati chafu.
Awali Wananchi hao wamepatiwa Elimu juu ya Matumizi sahihi ya Nishati ya Gesi Ili kuepukana na madhara ya kulipuka Kwa Moto kunakotokana na Matumizi yasiyo sahihi ya Nishati, Elimu hiyo imetolewa na Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Dodoma.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.