Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeipongeza Halmashauri ya Chamwino Kwa kuonyesha na kusimamia thamani ya fedha katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya elimu katika Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Justin Nyamoga ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya elimu ambapo Kamati hiyo ilitembelea katika Shule ya Sekondari Wasichana Manchali na Shule ya Msingi Membe.
“ukipita utaona thamani ya fedha inaonekana katika miradi hii, fedha iliyoletwa inaendana na matokeo tunayoyaona kwahiyo Kamati inawapongeza wote Kwa usimamizi mzuri wa miradi”
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe.Festo Dugange, amesema ofisi yake imepokea maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Kamati hiyo na kuyasimamia katika Halmashauri mbalimbali Nchini.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.