• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BAJETI YA OR-TAMISEMI 2017/2018 YAWASILISHWA BUNGENI

Imewekwa: April 18th, 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amewasilisha makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 Bungeni mjini Dodoma.

Akiwasilisha makadirio ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Simbachawene amesema jumla ya shilingi 6,023,559,414,000 zitatumika katika mwaka 2017/18 ambapo itahusisha mishahara, matumizi ya kawaida na utekelezaji wa iradi ya Maendeleo kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tume ya Utumishi wa Walimu, Mikoa na Halmashauri.

Kuhusu mafanikio ya TAMISEMI, amesema hadi kufikia Machi, 2017 jumla ya Halmashauri 177 kati ya 185 sawa na asilimia 96.2 zinatumia mfumo wa kielektroniki ambao umeboresha ufanisi katika ukusanyaji wa mapato. 

Pia migogoro ya ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa imeundiwa timu ya wataalamu inayoshirikisha Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Maliasili na Utalii, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Maji ili kupata njia bora ya kumaliza migogoro.

Kwa upande wa wafanyakazi hewa amesema, “jumla ya watumishi 13,369 ambao ni watoro, wastaafu na waliofariki wameondolewa katika orodha ya malipo ya mishahara ya Serikali”,  ambapo watumishi 541 walikuwa wa Sekretarieti za Mikoa na watumishi 12,828 wametoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, shilingi bilioni 2.7 zimerejeshwa Serikalini na pia waliohusika na upotevu huo wamechukuliwa hatua.

Pia, Ofisi ya Rais TAMISEMI imekamilisha ufungaji wa Tovuti katika Mikoa 26 na Halmashauri 185 ili kuwawezesha Wadau mbalimbali kupata taarifa na kufahamu majukumu yanayotekelezwa katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, sambamba na hilo mafunzo ya tovuti yametolewa kwa  Maafisa habari na TEHAMA wa Mikoa na Halmashauri zote juu ya matumizi yaliyokusudiwa ili kuhabarisha Watanzania masuala yanayotekelezwa na Serikali pamoja na kuimarisha Utawala Bora.

Katika mwaka 2017 katika shule za msingi wanafunzi wapatao 3,188,149 wameandikishwa kuanza darasa la Awali na Darasa la Kwanza sawa na ongezeko la wanafunzi 319,849 ikiwa ni matokeo ya Mpango wa Serikali wa utoaji wa Elimumsingi bila malipo unaotoa fursa kwa watoto wengi kupata elimu.

Aidha, Serikali imelipa madeni ya walimu yasiyo ya Mishahara kiasi cha shilingi bilioni 10.05, ununuzi wa vifaa vya Elimu Maalum shilingi bilioni 4.2, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Shule za Msingi 19 kwa shilingi bilioni 1.75.

Mhe. Simbachawene amesema, Halmashauri 184 zimetenga shilingi bilioni 56.8 kutokana na mapato ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Vijana na Wanawake. Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya ujasiriamali vya Vijana na Wanawake ili kukuza kipato na ajira.

 Amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Taasisi zilizo chini yake, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatarajia kukusanya shilingi 713,187,789,615 zitakazotokana na mauzo ya vifaa chakavu na nyaraka za zabuni, faini mbalimbali, marejesho ya masurufu na mishahara, ikiwemo kodi na ushuru kwa upande wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kulingana na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Chamwino Yaweka Mikakati Kuhakikisha Wanafunzi Wanamaliza Mzunguko Wa Elimu

    May 28, 2025
  • Wamiliki Mashine Za Kusaga Nafaka Wahimizwa Kufunga Vinyunyizi Vya Virutubisho

    May 26, 2025
  • Mchengerwa Awataka Maafisa Habari Kuhakikisha Wananchi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • Miche 350 Ya Matunda Yapandwa Kuadhimisha Kampeni Ya "Mti Wangu Birthday Yangu"

    May 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.