Wadau wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia wakiambatana na watalaam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wizara ya Afya na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI jana tarehe 28 Februari, 2025 wametembelea mradi wa ujenzi wa vyoo na kichomea taka katika Zahanati ya Humekwa iliyopo kata ya Haneti kijiji cha Humekwa, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Ziara hiyo ililenga kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Mpango Endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSSP) kupitia fedha za Lipa kwa Matokeo (PforR) zinazotolewa na Benki ya Dunia ili kufanikisha miradi ya Maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.