Leo tarehe 16.07.2019 Afisa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Filbert Mazige ameendelea kuwatembelea wafanyabiashara na wawekezaji ili kutoa elimu na kufuatilia mwenendo wa ulipaji wa mapato ya Halmashauri.
Akiwa ameambatana na Mtendaji wa Kata ya Manchali Ladislaus Loboto pamoja na Mtendaji wa Kijiji cha Wilunze Georgina Lusasi wametembelea makampuni mawili ya Mwitula na Steco wanaojishughulisha na uandaaji wa kokoto. Pia wamemtembele mwekezaji ambae anatarajia kuanzisha kiwanda cha juisi ya UBUYU eneo la Chalinze Nyama.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wameahidi kutoa ushirikiano kwa kulipa ushuru wa Halmashauri kwa wakati.
Bwana Mazige anatoa wito kwa wafanyabiashara kuja kuwekeza Chamwino katika sekta ya ARDHI, KILIMO na VIWANDA.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.