Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwa tarehe 24 Novemba 2019 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Utafanyika.
Waziri Jafo ameyasema hayo jana alipokuwa akifanya kikao na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na wadau wengine, kikao hicho kilifanyika kwenye Jengo Wizara ya TAMISEMI lililopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma na kurushwa mubashara na kituo cha televisheni cha TBC.
Aidha Mhe. Waziri ameeleza kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa bora kwa sababu kanuni za uchaguzi zimeandaliwa kwa kuwashirikisha wadau hivyo zitatatua changamoto zilikuwa zikijitokeza awali.
Chanzo: Matangazo Mubashara TBC
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.