• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Waheshimiwa Madiwani Chamwino Waridhia Kuanzishwa Kwa Mfuko Wa Elimu

Imewekwa: January 30th, 2025

Katika mapambano ya kuongeza ufaulu na elimu bora kwa wanafunzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo tarehe 30 Januari, 2025 Waheshimiwa Madiwani kupitia Mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya pili ya mwaka 2024-2025 wameridhia kuanzishwa kwa mfuko wa elimu Chamwino.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ukiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Edson Sweti ulipitisha ajenda hiyo iliyowasilishwa na katibu wa Baraza hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Tito P. Mganwa.

Akizungumza kabla ya kuridhiwa kwa ajenda hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Tito P. Mganwa amesema mfuko wa elimu ni suala la mkakati wa kitaifa kwa kila Halmashauri kuwa na mfuko wa elimu.

“Suala la uanzishwaji wa mfuko wa elimu lina sura mbili la kwanza ni mkakati wa kitaifa kwa kila Halmashauri iwe na mfuko wa elimu ndio maana kulikuwa na rasimu ya uanzishwaji wa mfuko wa elimu ya mwaka 2010, kulikuwa na rasimu tena iliyokuja kuhuishwa  na kusainiwa na Mhe. Jafo mwaka 2021”. Amesema Ndg. Mganwa.

Akiendelea baada ya kuridhiwa kwa ajenda hiyo Ndg. Mganwa amehaidi kusimamia mfuko huo wa elimu ili kufanya kazi kama ulivyokusudiwa.

“Mimi pia kama katibu na Mtendaji Mkuu wa Baraza lenu nawaahidi kwamba tutasimamia na kuhakikisha kuwa mfuko unafanya kazi iliyokusudiwa ili zile changamoto zinazojitokeza kwemye masuala ya elimu ziweze kutatuliwa na  mfuko huu”. Alisema Ndg. Mganwa.

Aidha, kupitia mkutano huo wa Baraza la Madiwani Mhe. Edson Sweti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino amepongeza Idara za Elimu Msingi na Sekondari kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wàTaifa wa  kidato cha nne ya mwaka 2024 kwa kushika nafas ya 4 ukilinganisha na  matokeo ya mwaka 2023 na kupanda kwa nafasi 4 katika Mkoa wa Dodoma na kwa kushika nafasi ya 3 kàtika mtihani wa Taifa wa darasa la saba.

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Chamwino Yaweka Mikakati Kuhakikisha Wanafunzi Wanamaliza Mzunguko Wa Elimu

    May 28, 2025
  • Wamiliki Mashine Za Kusaga Nafaka Wahimizwa Kufunga Vinyunyizi Vya Virutubisho

    May 26, 2025
  • Mchengerwa Awataka Maafisa Habari Kuhakikisha Wananchi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • Miche 350 Ya Matunda Yapandwa Kuadhimisha Kampeni Ya "Mti Wangu Birthday Yangu"

    May 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.