Vijana wazalendo( NEW AFRICAN YOUNG FIGHTERS) wanaotembea kwa miguu kutoka Dar es salaam kwenda Kagera kwenye kilele cha wiki ya vijana pamoja na tukio zima la kuzima Mwenge wa Uhuru litakalofanyika mkoani Kagera, leo tarehe 15 septemba, 2022 wamefika Ofisi ya Halmashauri ya Chamwino na kupokelewa na Afisa Utamaduni na Michezo ndugu Achimpota na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Dkt. Semistatus Mashimba.
Vijana hao wameeleza lengo la matembezi yao ni kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpendwa mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayolifanyia Taifa letu, kama vile miundombinu katika Sekta ya Mawasiliano, Elimu , Afya, Umeme na mengine mengi mazuri.
Kauli mbiu matembezi yao ni " TUJITOKEZE KUCHANGIA DAMU ILI KUOKOA MAISHA YA MAMA ZETU WANAPOJIFUNGUA NA WANAOPATA AJALI", ALIPO MAMA NA VIJANA TUPO.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.