Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino yasaini Hati ya Makubaliano ya awali na "Purandare Industries Tanzania LTD” kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha sukari katika Kijiji cha Dabalo, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Tukio hilo lilifanyika katika ukumbi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino tarehe 11/08/2017. Ilisisitizwa kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utanyanyua thamani ya zao la Miwa kwa wakulima katika kijiji cha dabalo pamoja na mkoa wa Dodoma kwa ujumla.
Kiwanda hiki kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha Tani 5,000 za Sukari kwa mwaka kwa kuanzia, matarajio ni kuzalisha tani 15,000 kwa mwaka. Kitatoa Ajira kwa watanzania wasiopungua 2,000, pia kitaongeza idadi ya Wakulima watakaokuwa wakizalisha Miwa Zaidi ya Wakulima 3,000.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.