Waziri wa Maji Aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji DabaloMheshimiwa Jumaa Aweso Waziri wa maji ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Kata ya Dabalo wilayani Chamwino,leo Julai 15, 2022. Mradi huu umetekelezwa kwa kutumia teknojia mpya ya matenki kutoka PLASCO na umegharimu zaidi ya shilingi milioni 900.Uwekaji huo wa jiwe la msingi ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi Mhe. Deogratius Ndejembi ambaye mradi huo upo katika Jimbo lake la Chamwino.Ilielezwa kuwa Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan yupo kazini kumtua mama Ndoo kichwani.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.