Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewaagiza wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanaanza maandalizi kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hapo mwakani.
Mhandisi Nyamhanga ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma wakati wa kuelezea tathimini ya matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2020 ambapo ufaulu wake umekuwa asilimia 82.68.
Amesema viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri wakishirikiana na wadau wa elimu wanatakiwa kuhakikisha miundombinu, samani na kuweka mazingira mazuri yakuwapokea wanafunzi wote watakaochaguliwa kuanza kidato cha kwanza Januari 2021.
“Kwa sasa tuko katika mchakato wa kuchagua wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza januari 2021, hivyo viongozi waanze kuweka mazingira ya kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanasajiliwa shuleni bila vikwazo vyovyote ili kutekeleza sera ya elimumsingi bila malipo” Amesisitiza Nyamhanga.
Amewakumbusha wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaadikishwa na kuhudhuria kikamilifu darasani.
Aidha, Mhandisi Nyamhanga ametumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri kukamilisha maandalizi yote yanayotakiwa kwa ajili ya uandikishaji wa wanafunzi wa shule za awali na darasa la kwanza watakaoanza masomo Januari 2021.
Hata hivyo, Mhandisi Nyamhanga amepongeza Mikoa mitatu ya Simiyu, Mara na Lindi amabayo wastani wa ufaulu umekuwa ukiongezeka kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo matokeoya Elimu ya Msingi.
Mkoa wa Simiyu ufaulu umekuwa ukiongezeka kutoka wastani wa asilimia 70.65 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 91.98, huku Mara ikiongeza wastani wa ufaulu kwa asilimia 63.68 mwaka 2018hadi kufikia asilimia 77.98 mwaka 2020 huku Lindi imeongezeka kutoka asilimia 68.71 mwaka 2018 hadi kufikia asolimia 82.25 mwaka 2020.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.