Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Leo tarehe 12 Oktoba 2019, amejiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga kura la Kitongoji cha Sokoine Chamwino Ikulu kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2019.
Akizungumza baada ya kujiandikisha yeye na Mke wake Mama Janeth Magufuli, Rais amesema kuwa baada ya ziara ya mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi ameamua kuja na Mke wake kujiiandikisha nyumbani Chamwino.
Aidha Mh. Rais ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye maeneo yao kabla ya Tarehe 14 Oktoba 2019.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.