“Hongereni Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kupata hati safi ya ukaguzi mwaka 2017/2018.”
Kauli hiyo imetolewa Leo Julai 1, 2019 na Bw. Chambi Sasamka Mkaguzi Mkuu wa Nje kutoka ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Dodoma kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Serikali ya Kijiji cha Chamwino Ikulu.
Katika kikao hicho, Baraza la Madiwani limepitia na kuidhinisha majibu ya hoja 47 ambazo zimejibiwa na tayari hoja saba zimefungwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mh. Samwel A. Kaweya amewataka Madiwani kushirikiana na watendaji ili kuhakikisha kila mwaka Halmashauri inapata Hati Safi na kuendelea kupata fedha za miradi (LCDG) zinazotolewa na serikali.
Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. Deogratius Philbert akiwasilishwa majibu ya Hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bw. A. H. Masasi akitoa ufanunuzi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.