• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AZINDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA IKOMBO, WILAYANI CHAMWINO

Imewekwa: January 27th, 2021

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa S.Kemikimba amezindua Mradi wa maji wenye Gharama ya Tshs 318,888,222/= kwa jitihada za Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Water Mission Tanzania  pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Ikombo Wilayani Chamwino hivi karibuni.


Taarifa  iliyosomwa na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Chamwino Mhandisi Christina Msengi imesema mradi huo ulilenga kuwapatia Maji safi na salama wananchi wa Kijiji hicho  ili kuepuka adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.


Kukamilika kwa Mradi huo ni jitihada  za Serikali ya Awamu ya tano chini ya Mhe.Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kupitia RUWASA kuchimba kisima kirefu kwa Tsh 25,000,000 katika bajeti ya 2017/2018, Shirika la Water Mission Tanzania likajenga miundombinu ya usambazaji Maji ya mradi huu kwa gharama ya Tsh. 288,726,222 na Mchango wa Wananchi kuwa Tsh 5,162,000.
"Kwa sasa mradi huu unahudumia watu wapatao 4,047 kati ya 4172  sawa na asilimia  97%. ya kijiji chote, aidha kisima hicho kina uwezo wa kutoa lita 23,400 kwa saa na kuendeshwa kwa mfumo wa nishati ya jua licha ya kuwa na mfumo wenye uwezo wa kutumia Nishati ya Umeme na Upepo (Multipurpose)" Mhandisi Christina. 
Akizungumza kwa niaba ya Shirika hilo, Mkurugenzi wa Shirika la Water Mission Tanzania  Benjamin Filskow alisema mradi huo ni alama ya mahusiano baina ya Serikali ya Tanzania, Shirika Water Mission na wananchi wa Kijiji cha Ikombo, akaeleza umuhimu wa kuilinda mradi huo na kuikumbusha Jumuiya ya Watumiaji Maji kuwa na matumizi mazuri ya fedha inayopatikana katika mradi huo na  akatoa pongezi kwa Wilaya ya Chamwino kusimamia Vizuri miradi ya Maji. 


Mapema kabla ya kumkaribisha  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji (Mgeni Rasmi), Remidius Emmanuel Afisa Tarafa Itiso ambaye katika tukio hilo alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Vumilia Nyamoga pamoja na kutoa shukrani kwa Shirika la Water Mission, kiongozi huyo alisema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaojaribu kuharibu miundombinu  ya Maji na akaahidi kupokea maelekezo yote kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji kupitia tukio hilo, akamaliza kwa kufikisha salaam za Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Deogratius Ndejembi ambaye Maji imekuwa ni sehemu ya kipaumbele chake.


Akitoa hotuba yake kwa Wananchi wa Kijiji cha Ikombo kabla ya kuzindua rasmi mradi huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa alisema kutekelezwa kwa miradi hiyo ni sehemu ya kutimiza malengo ya Serikali ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kupitia Sekta ya Maji upande wa Vijijini na  kwamba ifikapo Mwaka 2025 tunatakiwa tuwe tumehudumia wananchi kwa zaidi ya Asimilia 95 (lengo la kitaifa), akasisitiza mpango huo ni kwa maeneo yote, na hivyo viongozi ngazi zote watekeleza mpango huo kupitia maeneo yao.
Aliwashukuru sana Water Mission kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika Sekta hii muhimu ya maji na kuwapongeza Wananchi wa Ikombo kwa kuupokea vizuri mradi huo pamoja na kushiriki kikamillifu kuchangia nguvu  kazi  na kwa kufanya hivyo wananchi hao wameelewa malengo na nia  ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli. 
" Ni lazima kuwa na mipango endelevu ya kuhifadhi mradi huu, mtunze miundombinu, makusanyo mpate taarifa zake na RUWASA muwe karibu kukagua taarifa hizo, mpange miradi ya maendeleo kutokana na mradi huu wa maji" Mhandisi Nadhifa.


Alipongeza hatua ya Shirika la Water Mission kutoa mafunzo kwa Vijana kijijini hapo juu ya namna kuendesha mitambo ya kusukuma maji lakini akasisitiza iandaliwe miongozo maalum ya  matumizi ya mitambo hiyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikombo  Juma Madeje alisema kukamilika kwa mradi huo kumewezesha wananchi wa Kijiji hicho kutumia muda mwingi katika shughuli za maendeleo tofauti na zamani kabla ya mradi huo na sasa wanapata Maji Safi na Salama.



Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.