Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mhe. Deo Ndejembi jana tarehe 12 Disemba 2020, amefanya ziara kata ya Chilonwa, Msanga, Chamwino, Buigiri na Manchali na kukutana na Viongozi wa Kata na Vijiji hivyo pamoja na Bodi za shule za Sekondari kwa lengo la kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wa Kidato cha Kwanza wanaotarajiwa kuanza masomo mwezi Januari mwakani wanapata vyumba vya kutosha vya madarasa pamoja na viti na meza.
Mhe. Ndejembi amesisitiza kuwa mtoto anatakiwa kujengewa Mazingira bora ya kusomea ili aipende shule.
Kwa upande wa Viongozi hao wamemuahidi Mhe. Ndejembi kuwa maagizo yote aliyoyatoa watayatekeleza kwa wakati ili ifikapo Januari mwakani wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza wanapata madarasa ya kusomea.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.