KATIBU TAWALA NYALEGE AONGOZA KIKAO TATHIMINI YA UTENDAJI KAZI NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI.
Katibu Tawala Neema Nyalege wa Wilaya ya Chamwino ameongoza kikao cha tathimini ya utendaji kazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na kusikiliza changamoto zao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino leo Agosti 20, 2024.
Akizungumza na wajumbe waliohudhuria kikao hicho Katibu Tawala Nyalege amehimiza mashirika hayo yasiyo ya kiserikali yanayofanya shughuli zake katika Wilaya ya Chamwino kutanua wigo wa maeneo ya kufanyia kazi ili kuweza kuwafikia wananchi wanaoishi pembezoni mwa wilaya ya Chamwino ili nao waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika hayo.
Pia amesisitiza kuboreshwa kwa mfumo wa utoaji taarifa ili kuendeleza mawasiliano mazuri kati ya mashirika hayo na wataalam kutoka Serikalini pamoja na kuboresha muundo wa utekelezaji wa kazi zao (NGO’s) na kuweka muda wa kufanya shughuli zao
Aidha, ameomba mashirika hayo kushiriki katika shuguli mbalimbali za Serikali kwa kutoa huduma na kusaidia katika utekelezaji wa shughuli hizo yakiwemo matukio kama vile Mwenge na matukia mengine ya maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.