• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Bajeti Yaridhishwa Utekelezaji Miradi Ya Kilimo Chamwino

Imewekwa: November 11th, 2023


Kamati ya Kudumu ya Bunge la Bajeti imeridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa Wilayani Chamwino ikiwemo mradi wa Bwawa la Membe na mradi wa Skimu ya umwagiliaji Chinangali chini ya Mradi wa Building Better Tomorrow (BBT)

Akizungumza Leo Novemba 11,2023 Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mbunge wa Kilindi Mkoani Tanga Mhe. Omary Kigua wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyoanzia Mkoa wa Dodoma na inatarajia kufanyika kwa siku saba katika Mikoa mingine tofauti tofauti ikiwemo Manyara, Arusha, Singida, Tabora ,Iringa na kukamilika katika Mkoa wa Mbeya, amesema ziara hiyo ina lengo la kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo.

“Tumeridhika na shughuli zinazoendelea hapa na kiasi cha fedha ambacho kimetumika hakika kinasadifu kwamba kazi mnaisimamia vizuri ". Ameeleza Mhe. Kigua.

Aidha, amewaomba wananchi wa Kata ya Membe kutoa ushirikiano kwa Serikali popote utakapo hitajika kwani mradi huo utakapokamilika utakwenda kuwainua kiuchumi wananchi wote waliopo maeneo jirani na maeneo hayo ya miradi kwa  kuwa wao ndio watakuwa wanufaika  wa kwanza na hiyo ndiyo dhamira ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuinua maisha ya wananchi wa kipato cha chini.

Kwa Upande Wake, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ametumia fursa hiyo kuelezea azma ya Serikali katika kuhakikisha wanamuwezesha mkulima kuzalisha kipindi chote cha mwaka  bila kutegemea mvua.

“ Lengo letu kama Wizara tunataka Wananchi waweze kufanya shughuli za Kilimo mara mbili hadi tatu kwa mwaka wasitegemee mvua , Pia  mradi huu  hautakua kwa ajili ya kilimo tu bali hata wafugaji  watatengenezewa banio kwa ajili ya kunyweshea ng'ombe na shughuli za uvuvi pia zitafanyika.” Amesema Silinde

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amemshukuru Mhe. Rais kwa kufanya Mapinduzi ya Kilimo ndani ya Mkoa huo ambayo yatasaidia kuondoa njaa ,udumavu na kitakuwa chanzo cha uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Ameahidi kuendelea kuwa karibu na wakandarasi ili fedha zilizotolewa na Serikali ziweze kufanyiwa kazi husika kama ilivyokusudiwa na kwa ufanisi .

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Chamwino Yaweka Mikakati Kuhakikisha Wanafunzi Wanamaliza Mzunguko Wa Elimu

    May 28, 2025
  • Wamiliki Mashine Za Kusaga Nafaka Wahimizwa Kufunga Vinyunyizi Vya Virutubisho

    May 26, 2025
  • Mchengerwa Awataka Maafisa Habari Kuhakikisha Wananchi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • Miche 350 Ya Matunda Yapandwa Kuadhimisha Kampeni Ya "Mti Wangu Birthday Yangu"

    May 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.