Kamati tendaji ya baraza la biashara Halmashauri ya wilaya ya Chamwino limepatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo na ufanisi, Agosti 12, 2022 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Buzwagi uliopo kata ya Chamwino.
Mafunzo hayo yameandaliwa na kutolewa na mradi wa Good financial Governance(Utawala bora wa fedha) unaotekelezwa na GIZ kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani, Uswisi na Umoja wa Ulaya
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kujenga uwezo wa kamati tendaji za mabaraza ya biashara ya wilayakatika kuendesha mabaraza ya biashara ya Wilaya.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa na Bw. Swabiri Khalid mkufunzi wa warsha kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.
Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Bw. Godfrey Mnyamale akifungua mafunzo hayo aliwaomba wajumbe wafuatilie mafunzo hayo vizuri ili wapate kinachowasilishwa kwa usahihi. Aidha aliwataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano kwa Halmashauri katika masuala ya biashara.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.