• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Jafo awataka watumishi wa Umma kujiunga Benki ya Mwalimu

Imewekwa: March 12th, 2021

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemami Jafo (Mb), amewataka watumishi wa  wa kada ya Ualimu na watumishi  wengine wa Umma kujiunga na Benki ya Biashara ya Walimu ijulikanayo kama “Mwalimu Commercial Bank’ ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na benki hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya kadi za Viza, Mwalimu mobile na Mwalimu Wakala, Mhe Jafo amesema  umefika muda kwa maafisa masoko wa benki hiyo kuwatembelea watumishi walimu na wasio walimu kwa ajili ya kuwashawishi waweze kujiunga na benki ya Mwalimu.

Amesema walimu wengi wakijiunga na huduma za benki hiyo kutaiwezesha kukua zaidi, kwani kundi hilo linakadiriwa kuwa na watumishi  laki tatu ambao ni asilimia 72.6 ya watumishi wote wa Umma.

‘Kutokana na wingi wenu huu lazima muone ipo haja sasa ya kujiunga kwa wingi, lakini msiishie hapo tu, bali pia wafikieni watumishi wengine wa kada zingine, nalisema hili kwani najua nguvu ya walimu nikubwa na hakuna lakuwashinda’ amesema Jafo

Waziri Jafo amekumbusha kuwa malengo ya kuanzishwa kwa benki hiyo yalikuwa ni kuwahudumia walimu kama wateja wao wakuu lakini kufikia sasa idadi ya walimu waliojiunga kupata huduma za kibenki ni 41,000 tu.

‘Hapa maafisa masoko mnakazi kubwa yakujenga uelewa wa pamoja ili watu wafahamu kwa mba hiki ni chombo chao’ amesema

Akizungumza kuhusu huduma mpya zilizoanzishwa na benki hiyo, Waziri Jafo amesema kuanzishwa kwa huduma hizo ni ishara kuwa huduma zitolewazo na benki hiyo zimeongezeka, hivyo ni jukumu la uongozi wa benki hiyo kuongeza hamasa na ushawishi kwa walimu na watumishi wengine wa umma kujiunga ili kufaidi huduma za benki hiyo.

Uanzishwaji wa huduma hizi, ni ishara kwamba mmeongeza wigo, hata mtu ambaye alikuwa ansita kujiunga na benki yenu, sasa mmepata suluhisho kwani kupitia huduma kama ya Mwalimu Mobile mtu ataweza kufanya muamala eneo lolote.  

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.