Idara ya Elimu Sekondari Waweka Mikakati Kuondoa Daraja Sifuri
Watumishi wa Idara ya Elimu Sekondari makao makuu ya Halmashauri, mthibiti ubora wa Wilaya na Wakuu wa shule wamefanya kikao leo, Septemba 08, 2022 kujadili na kuweka mikakati mbalimbali itakayosaidia kuinua ufaulu wa wanafunzi wenye madarasa yenye Mitihani ya Taifa, hususani kidato cha nne na cha pili na kuondokana na ufaulu wa daraja sifuri.
Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri, ambapo wakuu wa shule wametakiwa kuhakikisha masomo yatakayofundishwa kwa muda wa ziada yafuate sheria kanuni na taratibu za nchi, ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama wa wanafunzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.