Hospitali ya Uhuru imeanza kufanya upasuaji mkubwa, na Septemba 4, 2023 umefanyika upasuaji kwa mara ya pili ambapo amepatikana Mtoto wa kike. Mama na Mtoto wote wako salama.
Taarifa hii imetolewa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Chamwino Dkt. Eusebius Kessy kwa menejimenti ya Halmashauri ya Chamwino.
" Hospitali ya Uhuru leo Septemba 4, 2023 imefanya upasuaji mkubwa wa pili, ambàpo amepatikana mtoto wa kike, mama na mtoto wako salama." Alisema Dkt. Kessy
Menejimenti ya Halmashauri ya Chamwino wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Semistatus H. Mashimba wamepongeza na kuushukuru uongozi wa Serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji mkubwa kwenye ujenzi wa miundombinu na manunuzi ya vifaa tiba.
Aidha wameushukuru uongozi wa Mkoa kwa kuwezesha madaktari bingwa waliowajengea uwezo madaktari wa hospitali ya Uhuru.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.