Taasisimya Foundation for Disabilities mkoa wa Dodoma imekabidhi vifaa kwa ajili ya walemavu wasioona pamoja na wenye ulemavu wa ngozi.
Makabidhiano hayo yamefanyika Ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Dkt. Semistatus H. Mashimba, leo Desemba 12, 2022.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ndugu Maiko Salali amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni mashine ya kuandikia wasioona yenye thamani ya shilingi milioni mbili na fimbo kwa ajili ya wasioona, pamoja na mafuta kinga kwa ajili ya wenye ulemavu wa ngozi zaidi ya chupa mia moja.
Aidha wameahidi kuendelea kuleta vitu hivyo kadiri watavyokuwa wanavipata.
Mkurugenzi Mtendaji amewashukuru wawakilishi wa Taasisi hiyo kwa msaada wao kwa kuwatambua watu wenye ukemavu wa wilaya ya Chamwino. Akiwahakikishia kuendeleza ushirikiano uliopo jati yao na kuahidi na vifaa wakivyovikabidhi vitakuwa salama na vitafika kwa walengwa
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.