Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kupata hati safi katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa hesabu zilizoishia Juni 30,2023.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Juni 19, 2024 Wilayani Chamwino Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezipongeza Halmashauri zote za Mkoa huo kwa juhudi zake katika kupunguza hoja za Mkaguzi na kupata hati safi.
" Sasa hivi Mkoa wa Dodoma wote umepata hati safi, tunategemea sasa ni mwendo wa hati safi kwa Halmashauri zote. kazi yetu kubwa ni kuendelea kupunguza zile hoja ndogo ndogo za Mkaguzi ili nazo ikiwezekana kama siyo kuzimaliza basi zipungue kwa kiwango kikubwa" Ameeleza Mhe. Senyamule.
Kwa upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amewasihi Menejimenti ya Wilaya kumtumia vizuri mkaguzi wa ndani kila anapotoa taarifa za kila robo ya Mwaka wa fedha ili kupunguza hoja kwa Mkaguzi Mkuu.
Kadhalika Mhe.Senyamule, Katibu Tawala Mkoa Bw.Kaspar Mmuya kwakuambatana na Uongozi wa Wilaya hiyo kutekeleza kauli mbiu ya " kero yako wajibu wangu" wamesikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kijiji cha Msanga kilichopo Wilayani humo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.