Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imetunukiwa vyeti viwili maalum kwa kuongoza na kuwa ya kwanza kitaifa kwa 90% ya uchanjaji wa chanjo ya UVIKO 19 na imeongoza kwa halmashauri za mkoa wa Dodoma kwa kuwa na matokeo yasiyoshuka katika utoaji wa chanjo hiyo.
Vyeti hivyo vimekabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwenye kikao cha tathimini ya utekekezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 na taarifa ya utekelezaji wa kampeni harakishi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO 19.
Kikao kilifanyika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Dodoma Alhamisi wiki hii.
Mkuu wa mkoa ameipongeza Halmashauri kwa kufanya vizuri kwenye zoezi hilo la utoaji wa chanjo ya UVIKO 19.)
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.