Magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni pamoja na shinikizo la juu la damu, kisukari, saratani, na magojnwa ya moyo yamekuwa chanzo cha vifo vingi, huku yakitajwa kuathiri zaidi watu wenye umri kuanzia miaka 30 na chanzo kikubwa cha magonjwa hayo kikitajwa kuwa 'mtindo mbaya wa maisha.'
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wilaya ya Chamwino Dkt. Emanuel Saidi, wakati wa kambi ya afya ya siku moja iliyofanyika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino jana Novemba 13, 2025 ikijumuisha utoaji wa elimu kuhusu magonjwa hayo pamoja na upimaji afya kwa watumishi katika kuadhimisha wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza.
“Zamani ilikuwa mtu akifikisha miaka 60, tunasema kwamba sasa huyu mtu ameingia kwenye uzee, mishipa imeanza kukakamaa anaweza kupata magonjwa yasiyoambukiza. Lakini sasa hivi, hata ukiwa mdogo ilimradi tu hujaweka mtindo wa maisha vizuri kuhusu namna unavyokula na kuishi unaweza kupata magonjwa yasiyoambukiza.”
Dkt. Emanuel amebainisha kuwa njia za kuepuka magonjwa hayo ni pamoja na kupata lishe bora, kufanya mazoezi, kupunguza matumizi ya pombe, kuepuka matumizi ya tumbaku, kufanya mazoezi na kuepuka mtindo mbaya wa maisha. Hata hivyo, amewaasa watumishi hao kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujua hali zao.
Mahudhurio ya kambi hiyo yaliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Tito P. Mganwa, na Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Bi. Prudence Kaaya ambao pia walliongoza watumishi kufanyiwa vipimo vya awali vya hali ya lishe, kisukari, shinikizo la juu la damu, homa ya ini, pamoja na upimaji wa hiari wa VVU/UKIMWI.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.