Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ni moja kati ya Halmashauri zitakazo nufaika na mradi wa SGR kwa wananchi wake wote waliopitiwa na mradi huo maeneo yao ya makazi.
Hayo yamesemwa leo tarehe 28 Disemba, 2020 na Bwana Dagobert Komba Mwezeshaji wa mafunzo wa Mpango wa kuwajengea uwezo Watumishi wa Halmashauri ya Chamwino kwa ajili yakuanza utekelezaji wa mpango wa urejeshaji wa maisha kwa wananchi wote waliopitiwa na mradi huo kwenye makazi yao.
Mkutano huo uliojumuisha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, una lengo la kuainisha shughuli zinazotarajiwa kufanywa kuhusiana na kuzuia au kupunguza athari za kijamii zitokanazo na ujenzi wa Mradi wa SGR kwa awamu ya I na ya II kwenye vijiji vya Igandu, Chimwaga, Mnase, na Msamalo Wilayani Chamwino.
Akifunga mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Ndugu Godfrey Mnyamale amesema kuwa, kutokana na unyeti wa mradi huo atachagua Wataalamu wenye uweledi wa hali ya juu kushirikiana na TRC katika kutoa elimu kwa Wananchi wa Vijiji vilivyopitiwa na mradi huo ili waweze kuwajengea uwezo Wananchi waliopitiwa na mradi huo kurejesha mfumo wa Maisha kama ilivyokuwa hapo awali.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.