• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Chamwino Kuhimiza Wakulima Kilimo cha Umwagiliaji

Imewekwa: August 12th, 2022



Katika kufikia azma ya Serikali ya awamu ya sita ya utekeleji wa ajenda ya kilimo ambayo inataka sekta ya kilimo kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030, Halmashauri ya wilaya ya Chamwino imeanza kutekeleza agenda hiyo kwa kuwahimiza wakulima kulima mazao mbalimbali ya umwagiliaji sambamba na ufugaji wa samaki ili kuifanya sekta ya hiyo kuwa ya biashara katika skimu ya umwagiliaji.

Bw.Godfrey Mnyamale ambaye ni mkuu wa idara ya kilimo,umwagiliaji na ushirika kutoka Halmashauri ya wilaya ya chamwino amesema hayo katika viwanja vya nane nane vilivyopo Nzuguni jijini Dodoma ikiwa ni siku chache tangu kumalizika kwa maonesho hayo Augost 10 mwaka 2022.

Akitolea ufafanuzi kuhusu kilimo cha umwagiliani jinsi ambavyo kinaweza kuleta tija kwa wakulima Bw.Mnyamale, anaeleza mikakati mbalimbali ambayo Halmashauri hiyo inafanya katika sekta ya kilimo kwa kushirikiana na wadau wa makampuni ya pembejeo ili kuleta manufaa kwa Watanzania na kuliongezea pato Taifa. 

Bw.Mnyamale anesema kuwa katika Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wameamua kushirikiana na wadau wa pembejeo pamoja na wakulima kwa ajili ya kujikita zaidi katika maeneo ya umwagiliaji ili waweze kulima mazao ya kutosha na kuuza mahindi mabichi ambayo yanafaida kubwa  kuliko mahindi makavu.

"Tunapenda kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya  uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia vitendea kazi na tumeshajipanga kwa kila afisa ugani kuhakikisha anahudumia wakulima wake ipasavyo kwa ajili ya kufikia malengo ya ajenda ya 2030 ambayo tunayaweka kama Taifa" amesema hayo Bw.Mnyamale.

Mbali na hayo Bw.Mnyamale amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeazimia kufikisha teknlojia ya kisasa katika kilimo na ufugaji mpaka vijijini ili wakulima waweze kunufaika na kilimo pamoja na mifugo. Naye mdau wa kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Bw.Onesmo Poteza ambaye ni bwana shamba wa mbegu za SEED-CO amewataka wakulima wote kulima kilicho cha kisasa ili kupata mazao bora kwa kutumia mbegu za kisasa.

  "Sisi kama wadau wa Halmashauri wa wilaya ya Chamwino tunaipongeza Halmashauri hiyo kwa kutupatia nafasi ya kuonyesha mbegu zetu katika maonesho haya ili wakulima waweze kuiona.

" Bw.Poteza mdau wa kilimo amesema kuwa Kuna mbegu ya tumbili 419 ambayo ni mbegu bora inayohimili magonjwa na  ukame ambayo tayari imeshaingia dukani.

Kwa upande wake mdau wa Kilimo kutoka Halmshauri ya Chamwino ambaye anajihusisha na uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali kutoka kampuni ya SEED OVER SEED amewataka Watanzania kutumia mbegu ambazo ni bora katika kilimo. Akizungumzia mbegu ambazo zinazalishwa na kampuni ya SEED OVER SEED ameeleza mbegu zinazopatika katika kampuni hiyo ikiwemo mbegu ya kabichi ambayo inaweza kukomaa kwa siku 75 na kufikia uzito wa kilo 6 hadi kilo 10 pamoja na mbegu ya pilipili hoho, maharage lishe ambayo yana madini ya Iron na madini ya zink.Amesema ni mbegu bora ambazo zinauwezo wa kumfanya mkulima akalima na kuvuna kwa haraka bila kupata hasara kwani mbegu hizo ni himilivu.

  "Tuna maharage lishe ambayo yameongezewa virutubisho vya aina  mbalimbali  ikiwemo madini ya Iron pamoja na Zink ambayo yanaimarisha mifupa pamoja na macho ambayo yaliletwa kwa  ajili ya kuepusha ulemavu kwa watanzania nchi nzima"  

Maonesho ya siku kuu ya wakulima nane nane mkoani Dodoma yalifanyika katika viwanja vya  Nzuguni Jijijni hapa ambayo yalifunguliwa na kuhitimishwa na mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, ambapo katika maonesho hayo Halmashauri ya wilaya ya Chamwino imefanikiwa kupata mshindi wa kwanza katika kundi la wakulima bora wa kilimo cha kutegemea mvua Bw.ALISENI DAMIANI ambaye alipatiwa hati ya ushindi huku pia  Halmashauri ya wilaya ya Chamwino ikipatiwa hati ya mshindi wa tatu katika kundi la Halmashauri za mkoa wa Dodoma.                           

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.