Swahili
  • English
  • Swahili
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo Kijiji cha Manzase

Imewekwa: June 16th, 2017

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amewataka wananchi wa kijiji cha Manzase, kuhakikisha kuwa wanautunza mradi wa maji ulioanzishwa kwa gharama yoyote.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Manzase Wilaya ya Chamwino, wakati wa ziara aliyoifanya ya  kukagua  mradi wa maji Mheshimiwa Jaffo alisema iwapo wananchi hao watautunza mradi huo vizuri utawasaidia zaidi kwani wamepata taabu ya maji kwa kipindi kirefu sana.

“ Kumekuwa na kawaida ya baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo miradi ya namna hii imekuwa ikianzishwa kwa makusudi kabisa, wanaiharibu miundo mbinu ya miradi hii kwa kukata mabomba kwa makusudi  kwa lengo la kunywesha mifugo, kuiba vifaa mbali mbali kwenye mabomba na kuiba mitambo inayosaidia kusukuma maji” Alisisitiza Mhe. Jafo.

Aidha, aliwataka Viongozi wote wa kijiji hicho kuhakikisha kuwa kamati ya maji ya kijiji ambayo ndicho chombo maalumu cha kusimamia maji katika ngazi ya kijiji kinasimamiwa ipasavyo kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi hao kujimilikisha miradi hiyo kwa kutumia fedha zinazokusanywa kwa matumizi yao wenyewe, na pindi miundo mbinu inapoharibika kijiji kinakosa fedha za kupatra marekebisho.

Diwani wa kata ya Manzase Mh. Steven Kwanga alisema, mradi huo wa maji utasaidia sana katika ukuaji wa uchumi wa wananchi wake kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta huduma ya maji, vilevile wananchi wamekuwa wakitumia kiasi kikubwa cha fedha kununua maji badala ya fedha hiyo ingetumiwa kutimiza mahitaji mengine.

Mradi huo wa maji wa kijiji cha Manzase unatarajiwa kuzinduliwa wakati wowote mwezi huu kwani mkandarasi wa mradi huo akishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI amekwisha ukamilisha kwa kiasi kikubwa na unatarajiwa kuhudumia idadi ya watu wasiopungua 8000.

Katika ziara hiyo Mhe. Jafo alikuta Idadi kubwa ya watoto walioandikishwa kujiunga na darasa la kwanza hali iliyopelekea kukosekana kwa vyumba vya kutosha kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi ambapo kwa kutatua kero hiyo, shule hiyo imeanza ujenzi wa vyumba vya madarasa na kwa upande wake alichangia bati 164 ili kuwezesha madarasa hayo kukamilika.

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Mafunzo Ya Uboreshaji Wa Daftari La Wapiga Kura Awamu Ya Pili Yatolewa Chamwino

    May 14, 2025
  • Chamwino Waibuka Kidedea Tuzo Za MSD Kanda Ya Kati

    May 11, 2025
  • Kata, Shule Na Walimu Walioibuka Kidedea Kwa Ufaulu 2024 Wajizolea Vitita Chamwino

    May 10, 2025
  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.