• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA HOSPITALI YA UHURU

Imewekwa: December 6th, 2020

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amekagua umaliziaji wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru unaoendelea katika wilaya ya Chamwino, Dodoma na kuagiza huduma zianze kutolewa ifikapo Desemba 20 mwaka huu.


Amekagua hospitali hiyo leo (Jumapili, Desemba 6, 2020) na amesema vifaa vyote zikiwemo samani, vifaa tiba vinavyotakiwa kuwepo kwenye hospitali hiyo vipelekwe na vifungwe ili huduma zianze kutolewa.


“Tunakusudia kumuomba Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli aje kuzindua hospitali hii kabla ya Desemba 30 mwaka huu, hakikisheni vifaa vyote zikiwemo samani na vifaa tiba vinaletwa na kufungwa ili Desemba 20 huduma zianze kutolewa.”


Desemba 3 mwaka huu Rais Dkt. Magufuli aliahirisha maadhimisho ya sherehe za miaka 59 Uhuru zilizotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2020 na kuelekeza kiasi cha shilingi 835,498,700 zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za hizo zitumike kununulia vifaa mbalimbali kwa ajili ya Hospitali ya Uhuru.


Mbali na ununuzi wa vifaa hivyo, pia Rais Dkt. Magufuli aliagiza fedha hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kuzunguka eneo la hospitali hiyo pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingilia hospitalini hapo.


Hadi kufikia sasa ujenzi wa hospitali hiyo ya Uhuru umegharimu shilingi bilioni 4.2. Januari 2019 wakati akipokea gawio la hisa za kampuni ya Simu ya Airtel Rais Dkt. Magufuli aliagiza kiasi cha shilingi 2,415,151,650.00 zilizotolewa na kampuni hiyo zitumike katika ujenzi wa hospitali hiyo.


Novemba 20, 2018, Rais Dkt. Magufuli aliagiza kiasi cha sh. 995,182,000.00 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru zitumike kujenga Hospitali ya Uhuru, ambayo kwa sasa ujenzi wake upo katika hatua za umaliziaji.


Kauli mbiu ya maadhimisho ya 59 ya Uhuru kwa mwaka huu inasema; ‘Miaka 59 ya Uhuru na Miaka 58 ya Jamhuri: Tanzania yenye Uchumi Imara Itajengwa na Watanzania Wenyewe, Tufanye Kazi kwa Bidii, Uwajibikaji na Uadilifu.’


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge aliishukuru Serikali kwa uboreshaji wa huduma za afya mkoani Dodoma ukiwemo ujenzi wa hospitali hiyo ya Uhuru, ambapo ameiomba iwaongezee wataalamu wa afya.


Alisema mahitaji ya wataalamu wa afya wakiwemo madaktari katika mkoa ni 2,505 huku waliopo ni wataalamu 1,767, hivyo ameomba Serikali iwasaidie kutatua changamoto hiyo kwa kuajiri wataalamu wa kutosha katika sekta hiyo.


Pia, Dkt. Mahenge amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba za wataalam, ambapo aliomba msaada wa ujenzi wa nyumba hizo ili kuwawezesha watoa huduma hao kuwa na makazi karibu na hospitali.



Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Chamwino Waibuka Kidedea Tuzo Za MSD Kanda Ya Kati

    May 11, 2025
  • Kata, Shule Na Walimu Walioibuka Kidedea Kwa Ufaulu 2024 Wajizolea Vitita Chamwino

    May 10, 2025
  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.