• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Watakaoshindwa kukamilisha zoezi la kupandisha watumishi madaraja kuchukuliwa hatua - Prof Shemdoe

Imewekwa: June 17th, 2021

-Dar es Salaam

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe amesema atachukua hatua kwa viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi la ubadilishwaji wa kada na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wote walio chini ya OR-TAMISEMI, na kuagiza zoezi hilo kukamilika ndani ya siku moja ya ziada.

Profesa Shemdoe alitoa agizo hilo leo Juni 17, 2021 alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo ambapo pamoja na mambo mengine aliwasisitiza wale wote waliopewa dhamana ya kufanikisha suala hilo kukamilisha haraka, ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Sintokuwa tayari nipoteze kazi kwa sababu ya uzembe wa mtu, kila halmashauri inapaswa kukamilisha kazi hiyo ifikapo kesho, nasisitiza kuwa wale ambao  bado hawajakamilisha kazi hiyo hadi hivi sasa kuhakikisha wanaliza kabla ya hatua zingine,” alisisitiza Profesa Shemdoe.

Alieleza kuwa hadi kufikia jana Juni 16, 2021 asilimia 80 ya watumishi 239,000 kutoka mamalaka zote  za Serikali za Mitaa walikuwa tayari wameshaingizwa katika mfumo huo huku asilimia 20 iliyobaki ikitarajiwa kukamilishwa Juni 16-17, 2020 tayari kwa utekelezaji wa agizo hilo la Rais Samia.

Aidha alizipongeza Halmashuri zote zilizopambana kwa kujitoa usiku na mchana kufanikisha zoezi hilo, na zaidi pongezi hizo akizielekeza kwa uongozi na timu ya maafisa utumishi wa Jiji hilo la Dar es Salaam kwa ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa jukumu hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo Bernadetha Mwaikambo, hadi kufikia jana watumishi 2555 kati ya 2625 walikuwa tayari wameshaingizwa katika mfumo huo wa upandishwaji vyeo na kwamba idadi ya watumishi 70 waliosalia kutokuingia kwao kumetokana na changamoto mbalimbali ambazo Katibu Mkuu huyo wa Tamisemi amesema atazifanyia kazi.

Pia Profesa Shemdoe alisema kuwa awali zoezi la utekelezaji wa mfumo huo lilipaswa kukamilika Juni 12, 2021 lakini kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali walifanya mazungumzo na Wizara ya Utumishi, hatua iliyosaidia kuongezewa  muda kidogo ili kulikamilisha.

Alitoa msisitizo kwa maafisa hao kuhakikisha wanapaswa kuitumia fursa hiyo ya ziada iliyotolewa ipasavyo ili kukamilisha suala hilo vinginevyo watachukuliwa hatua za kitumishi.

Kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa umma Na 8 ya mwaka 2002, pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 na taratibu za uendeshaji za mwaka 2003, pamoja na miongozo na nyaraka mbalimbali zilizotolewa na Serikali, Mamlaka ya kupandisha vyeo watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa isipokuwa Walimu kwa mujibu wa Kanuni ya D. (f) na (g) ya Kudumu ya mwaka 2009 ni Halmashauri yenyewe.

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Wakuu Wa Shule Wapatiwa Mafunzo Ya Mfumo Wa NeST

    March 21, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.