• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mhe. Jafo Azinduwa Mradi wa Maji wa Kijiji cha Wilunze

Imewekwa: May 30th, 2017

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakandarasi nchini kutimiza wajibu wao na kutekeleza miradi wanayopewa na Mamlaka za Serikali nchini kwa wakati, uaminifu na kuacha ubabaishaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Mheshimiwa Jafo amesema mkandarasi yeyote atakayepewa tenda ya mradi katika halmashauri yoyote nchini na asiitekeleze kwa wakati hataweza kupewa tenda mahali popote pale nchini.

“Kumekuwa na uzembe kwa Wakandarasi nchini, mkandarasi anapewa kazi ya kujenga daraja, kujenga visima vya maji, barabara au mradi mwingine wowote katika halmashauri, badala ya kutekeleza mradi huo kwa wakati ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo, yeye analeta uzembe na ubabaishaji, mtu wa namna hiyo hatutamvumilia katika serikali hii” Alisisitiza, Mhe. Jafo.

Aidha, aliwataka wanakijiji wa Wilunze kuulinda mradi huo wa maji kwa kila mmoja kuwa msimamizi wa mradi na kuutaka Uongozi wa kijiji hicho kuhakikisha kuwa kinaundwa chombo cha watumiaji wa maji kijijini hapo ambacho kitakuwa na wajibu wa kusimamia mradi huo.

Mradi wa maji wa kijiji cha Wilunze uliozinduliwa leo ni mmoja kati ya miradi ya maji ya vijiji kumi inayojengwa wilayani Chamwino kupitia Programu ya Maji Vijijini. Mradi huo uliojengwa na Mkandarasi M/S Kijima Contractors akisimamiwa na Ofisi ya Mhandisi wa maji wilaya ya Chamwino umegharimu jumla ya sh. 347,909,621.

 Kwa upande wake Mbunge wa Chilonwa Mhe.Joel Mwaka amemshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri na  Serikali kwa ujumla kwa kuwapatia huduma ya maji safi wananchi wake na  kuwasisitiza wananchi kuuliunda mradi huo kwa hali na mali kwani umeigharimu Serikali kiasi kikubwa cha fedha katika utekelezaji wake

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Chamwino Waibuka Kidedea Tuzo Za MSD Kanda Ya Kati

    May 11, 2025
  • Kata, Shule Na Walimu Walioibuka Kidedea Kwa Ufaulu 2024 Wajizolea Vitita Chamwino

    May 10, 2025
  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.