• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu Wa Wilaya Chamwino Akabidhi Hati Miliki za Kimila Kwa Wakulima wa Chifukulo

Imewekwa: November 27th, 2018

 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Vumilia Nyamoga amekabidhi  hati miliki za kimila kwa wakulima wa maembe wa kijiji cha chifukulo hivi karibuni kwenye hafla iliyofanyika kijijini hapo.

Ilielezwa mradi huu wa kuandaa mpango wa matumizi  ya ardhi katika kijiji cha Chifukulo unafadhiliwa na kampuni ya Local Investiment Climate na mpaka sasa jumla ya hati miliki za kimila 175 zimeandaliwa na zimekamilika.

Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya amewataka wakulima kutokubeza uwekezaji huo wa shamba la maembe na badala yake ni vema kila kaya au familia ikawa na eneo kwenye shamba hilo, alisema ‘Isiwe ninyi mmetoa maeneo yenu ekari 500 kisha wao wakawa pembeni  na wakafaidika wa pembeni kitu ambacho kitakuwa  hakipendezi.’

Amewataka wayasimamie maeneo watakayopewa kwa uaminifu kwa kufuata kanuni za kilimo bora ili waweze kupata mazao mengi na watakapouza waweze kupata fedha za kujikimu na familia zao na kwa kufanya hivyo wana Chifukulo wana uhakika wa kuwa matajiri wa baadae. Amewaahidi wakulima kuwa kiwanda kitakapokuwa tayari na kwa kuwa ushirika tayari upo utawekwa utaratibu mzuri na bei ambayo itawanufaisha wakulima itawekwa

Alieleza kuwa kiwanda kwa ajili ya kusindika ‘juice’ kitakapojengwa maembe yaliyolimwa sasa hayataweza kukidhi mahitaji  ya kiwanda hivyo alisisitiza wasiuachilie uwekezaji huo.

Akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Afisa Ardhi Mteule ndugu Letare Shoo alisema mradi huu wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi , upimaji wa mashamba ya maembe umetumia Tshs. 52,538,900/=

Aidha alieleza kuwa maandalizi ya hati miliki nyingine yanaendelea ambapo wamiliki wa mashamba wanatakiwa kujaza fomu za utambuzi na kupigwa picha, zoezi ambalo linaendelea katika ofisi za LIC.

Vilevile alieleza kuwa kampuni ya ya LIC inafadhili uendelezaji wa shamba kwa kununua miche bora ya maembe ili ipandwe kwenye mashamba ya wanachama kwa lengo la kuboresha uzalishaji  na ununuzi  huo wa miche umegharimu kiasi cha Tshs. 37,500,000/=

Aidha ilielezwa kuwa katika kufanikisha ujenzi wa kiwanda katika eneo hili tayari hatua za awali zimeanza kutekelezwa kwa kuandaa andiko la mradi (business plan) kuainisha aina za mitambo itakayotumika, bidhaa zitakazozalishwa na michoro ya usanifu wa kiwanda.

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.