• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Katibu Tawala Dodoma Ateta na Watumishi Chamwino

Imewekwa: May 30th, 2024

Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Ndg: Kaspar Kaspar Mmuya amefanya ziara ya kikazi Wilayani Chamwino Mei 30,2024 kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuongea na watumishi.  

Akizungumza katika kikao kazi hicho amewapongeza kwa utendaji mzuri na kuwaelekeza kuwa waendelee kufanya kazi kwa tija na  kwa kufuata sheria kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo ya viongozi, pamoja na mila na desturi ya eneo wanalofanyia kazi.

 "Nawapongeza kwa sababu mnafanya kazi kwa upendo na kwa kujitoa kwa niaba ya Mheshimiwa Rais." Alisema.

Katika kutekekeza wajibu amewataka watumishi kujua wajibu wao unaoendana na vyeo vyao.

Vilevile amewaelekeza watumishi kutumia busara chanya yenye matokeo makubwa zaidi pale inapohitajika katika kutekeleza majukumu yao  kwa manufaa ya Umma na Taifa.

Amewataka watumishi kutoa huduma kwa haki na kusisitiza kuwa hapendi huduma inunuliwe. "Toeni huduma kwa kufuata haki na usawa." Alisema Katibu Tawala.

Katibu Tawala Mkoa amezungumzia pia suala la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ambapo amesema mapato yanapaswa kukusanywa vizuri na kurudisha kile kilichokusanywa kwa wananchi kwa kuwapelekea maendeleo.

" Mheshimiwa Rais anapotembea kwenye ziara zake anaangalia mbona ile hela ninayoambiwa na Kamishina wa kodi Alfayo Kidata haioni kwenye maisha ya watanzania? Alisema Katibu Tawala.

Vilevile amewaasa watumishi  kuhusu kuongeza kipato na uchumi wa familia na kuwasisitiza kupanda miti ya matunda kwenye makazi yao hata kwa wale wanaoishi kwenye nyumba za kupanga kwani kufanya hivyo hakutawaathiri chochote. Alitolea mfano mti mmoja wa parachichi unauwezo wa kukuzalishia mavuno ya wastani wa laki tatu kwa mwaka.

Amewaasa pia watumishi kupendana wanapokuwa kazini na wasipende kuwa na tabia za chuki na kupenda wenzao waharibikiwe. Ameeleza kuwa kuna watu furaha yao huwa ni kuona wenzao wanaharibikiwa.

"Muda mwingi tunautumia tukiwa kazini, ndugu yako mama yako, baba yako, rafiki yako ni watu hawa ambao wamekuzunguka. Inaniuma mno kuwa mimi bosi wangu simpendi au msaidizi wangu simpendi, au mtumishi wa chumba jirani simpendi. Kwa sababu ukichukia kuna seli fulani za mwili wako zinavunjika." Alisema.

"Unapoishi kwa upendo na mwenzako unamuongezea ari ya kufanya kazi na kwa kufanya hivyo tija inaongezeka. Watu wakiamka asubuhi wapende kwenda kazini." Alisema.

Watumishi pia wamekumbushwa wajibu wa kusikiliza kero za wanaanchi na kuzipatia ufumbuzi kama kaulimbiu ya mkoa inavyojielekeza inayosema "KERO YAKO WAJIBU WANGU"

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Wakuu Wa Shule Wapatiwa Mafunzo Ya Mfumo Wa NeST

    March 21, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.