• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Katibu Mkuu OR TAMISEMI Prof. Shemdoe atangaza ajira za Elimu na Afya

Imewekwa: June 26th, 2021

Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe ametangaza ajira za  Elimu 6,749 kwa shule za Msingi na Sekondari na Wataalamu wa Afya 2,726.

Akitoa Taarifa hiyo Jijini Dodoma mapema leo hii Prof. Shemdoe amesema waombaji wa kada ya Ualimu walikua 99,583  na Wataalam 37,437 wa kada ya afya, wakiwemo wenye ulemavu 1,099  waliomba nafasi hizo.

“Baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji wa maombi Walimu 6,949 (3,949 wa shule za Msingi na 3000 wa shule za sekondari) na Wataalam wa kada za afya 2,726 wamepangiwa vituo vya kazi” amesema Prof. Shemdoe

Ametaja vigezo vilivyotumika kuwapata watumishi waliokidhi sifa kuwa ni pamoja na Mwaka wa kuhitimu chuo ambapo waombaji waliomaliza mapema zaidi (mwaka 2012 hadi 2019) kulingana na mahitaji yaliyopo katika kada husika wamepewa kipaumbele.

Aidha, Umri wa mwombaji umezingatiwa kwa kutoa kipaumbele kwa  waombaji wenye miaka zaidi ya 40 ambao wamemaliza miaka ya mwanzoni kama ilivyobainishwa kwenye kipaumbele cha awali.

“Sababu ni kuwa kama hawataajiriwa mapema wakifikisha miaka 45 ambapo hawataweza kuajiriwa tena Serikalini kwa ajira ya masharti ya kudumu” amesema Prof. Shemdoe.

Pia waombaji waliofungana kwa sifa zilizobainishwa awali yaani mwaka wa kuhitimu na umri amepewa kipaumbele msichana/mwanamke, bila kuathiri uwiano wa asilimia 50 amefafanua.

Vile vile, Prof Shemdoe amebainisha kuwa endapo waombaji wamefungana kwenye sifa ya Mwaka wa kuhitimu, Umri na Jinsi basi amepewa kipaumbele mwenye umri mkubwa zaidi kwa kuangalia tarehe ya kuzaliwa.

Akitaja changamoto zilizojitokeza wakati wa uchambuzi na kusababisha baadhi ya waombaji kupoteza sifa amesema ni pamoja na Waombaji kutoweka kwa usahihi viambatisho vyote vinavyohitajika kwa mujibu wa tangazo la ajira, waombaji kutofuata maelekezo ya mfumo wa maombi ya ajira, Kutofautiana kwa taarifa za mwombaji alizojaza kwenye mfumo wa maombi ya ajira na taarifa zilizopo kwenye viambatisho pamoja na Waombaji kuandika taarifa zisizo sahihi kuhusu masomo anayoomba kufundisha na yaliyopo kwenye vyeti mafunzo au hati za matokeo.

Prof. Shemdoe ametumia fursa hiyo pia  kutoa maelekezo kwa  waajiriwa wapya kuwa wanatakiwa kuripoti kwa Wakurugenzi na kufanya kazi kwenye vituo walivyopangiwa na sio katika Makao Makuu ya Halmashauri.

‘Mwajiriwa mpya atakayechukua posho ya kujikimu na baadaye asiripoti katika kituo chake cha kazi alichopangiwa atachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sharia na taratibu’ amesema.

Ameongeza kuwa Wajiriwa wapya hawatabadilishiwa vituo vya kazi walivyopangiwa kwa kipindi cha miaka (3) na

wanatakiwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 14 Julai, 2021 na ambao hawataripoti kwa muda huo watakuwa wamepoteza nafasi zao na zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa waliopo kwenye Kanzi data (Database) ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

 Prof. Shemdoe amewataka waajiriwa wapya  kuripoti katika vituo vyao vya kazi wakiwa na Vyeti halisi vya Kidato cha Nne na Sita, Vyeti halisi vya kitaaluma vya kuhitimu mafunzo katika kada husika, Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho ya NIDA pamoja na

(Cheti halisi cha kuzaliwa.

Halkadhalika amewataka  Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo zimepangiwa waajiriwa wapya kuwapokea na  kuwawezesha   kwa   kuzingatia  sheria, kanuni,  taratibu   na miongozo  ya Utumishi wa Umma na  baadaye kutoa  taarifa ya uripoti wao katika Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaelekezwa kukamilisha taratibu za ajira haraka ili watumishi wapya waingizwe   kwenye   mfumo   wa   malipo   ya   mshahara (Payroll) mapema iwezekanavyo” alisisitiza Prof. Shemdoe

Majina ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz.

Tarehe 6 Aprili, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alitoa kibali cha ajira kwa kada za Ualimu na Afya kwa ajili ya kuajiri walimu 6,949 wa Shule za Msingi na Sekondari na wataalam wa Afya 2,726 na kibali hicho kilifuatiwa na tangazo la ajira la tarehe 9 Mei, 2021.

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Msisitizo Watolewa Mahindi Ya Bei Nafuu Yanayotolewa Na Serikali Kupelekwa Kila Kata

    May 08, 2025
  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.