• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Chamwino District Council
Chamwino District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadlili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Fedha
      • Mipango
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Mazingira
      • Ardhi Maliaasili na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Agricultuer
    • Mifugo
    • Fishing
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Afya Elimu na Maji
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
      • Ardhi
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopitishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Sheria Ndogo
    • Mikakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Chamwino Yaweka Mikakati Kukabiliana Na Maafa

Imewekwa: December 1st, 2023

Kamati ya Maafa Wilaya ya Chamwino imefanya kikao leo Novemba 30, 2023 kwa lengo la kuchukua tahadhari ya kudhibiti majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania ( TMA) ya uwezekano wa uwepo wa mvua za juu ya Wastani ( ElNino). Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

Katika kikao hicho Mtaalam kutoka TMA ndugu Joseph J. Mgumba aliakwa na aliweza kutoa elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu hali ya hewa ikiwemo suala la matarajio ya uwepo wa mvua za juu ya wastani kwa Wilaya ya Chamwino kuanzia mwezi Desemba 2023 hadi Februari 2024.

Vilevile mtaalam wa TMA aliweza kueleza kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kuokana na uwepo wa mvua nyingi kama vile magonjwa ya mlipuko, uharibifu wa miundombinu ya barabara na majengo, kukatizwa kwa usafiri wa anga, athari za uchumi na mazingira.

Kupitia kikao hicho kamati imeweza kujadili na kuweka mikakati mbalimbali itakayosaidia kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza katika kipindi hicho cha mvua.

Moja yamkakati ni TARURA kuimarisha miundombinu ya barabara na madaraja  husani kwenye maeneo muhimu ya mapato na sehemu za kutolea huduma za afya yaani zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Ilijadiliwa pia kuhusu wananchi kupewa elimu kuhusu kutibu maji na matumizi sahihi ya vyoo ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Suala jingine lililopewa kipaumbele ni kununua dawa za kutosha kwaajili ya tahadhari ya magonjwa ya mlipuko ili ukitokea ugonjwa matibabu yaweze kutolewa.

Kwamaeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi kama Ikowa, Ingunguli kuhakikisha dawa na chanjo  za kutosha zinanunuliwa na kupekwa vituo husika.

Kwaajili ya madhara ya ajali yanayoweza kutokea kutokana na athari za mvua kubwa  ni kuhakikisha kunakuwa na magari ya wagonjwa muda wote pamoja na timu za dharura zitakazoweza kufanya kazi. Ilielezwa timu za dharura zimewkwa kituo cha Afya Chamwino, Hospitali ya Uhuru, Mpwayungu, Haneti, Mlowa barabarani na kusambaza namba za kitengo cha dharura cha afya kilichopo mkoani ambacho kinafanya kazi masaa 24 kwa wananchi ili linapotokea jambo kufanya mawasiliano.

Kamati pia imejiwekea mkakati wa kuyatambua maeneo yenye viashiria vya kutokea maafa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na maafa nà namna ya kuchukua hatua pindi yanapotokea ikiwa ni pamoja na kuziamsha kamati za maafa za kata na kuwaeleza majukumu yao.

Pia kubainisha ya kuwahifadhi watu iwapo maafa yametokea na hivyo kupelekewa huduma kwenye eneo hilo.

Aidhà ilielezwa kuwa wadau watakaoweza kusaidia pindi majanga yanapotokea wanapaswa kubainishwa ili kuweka urahisi wa kujua nani asaidiè kipi pindi majanga yanapotokea.

Vilevile ilikubalika kuwa elimu itolewe kwa madereva wanaondesha vyombo vya moto vya usafiri ili wachukue tahadhari kwa kipindi hiki ili kuepusha maaafa kwani panapokuwa na mvua nyingi barabara zinakuwa na utelezi, ukungu na pengine kukatika kwa barabara pamoja na madaraja. Hivyo tahadhari inatolewa kwa waendesha vyombo vya usafiri chamwino ili kuepusha maafa ni heri kusitisha safari pindi wanapoona hali ya hewa siyo nzuri au madaraja yamejaa maji kwa kufanya hivyo watakuwa salama.

Mkakati mwingine uliowekwa ni pamoja na kuwashauri wananchi kupunguza matawi ya miti yaliyokarobu na nyomba zao ili miti hiyo isiangukie nyumba na kuzibomoa.

Kwa upande utekelezaji wa miradi ya maendeleo ilikubaliwa kuwa vifaavyote vinavyohitajika kwenye mradi vinunuliwe vyote mapema na kupelekwa site ili hata itakapotokea maafa yoyote miradi isikwame kutekelezwa.

Kwa upande wa kilimo Serikali chini yauongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani  suala la  uwepo wa mvua nyingi wanalichukulia kama fursa na ndio maana wamejenga bwawa kubwa pale Membe kwa ajili ya umwagiliaji litakalochukua maji yanayotoka sehemu mbalimbali yaliyokuwa yakileta maafa  mbalimbali kwa wananchi. Na kuna mpango mwakani wa kufanya ukarabati wa kuondoa tope kwenye mabwawa ya Manchali na Buigiri ambayo pia yatasaidia kupunguza maji yaliyokuwa yakifanya uharibifu.

Kutokana na uwepo wa maji mengi pia hupelekea ugonjwa wa ' riftvalley' kwa mifugo hivyo wafugaji na wananchi kwa ujumla waelimishwe pindi wanapoona mifugo inatoa mimba hiyo ni dalili mojawapo ya ugonjwa huo., hivyo watoe taarifa mapema mifugo ichanjwe kwani chanjo ni za bure.

Vilevile wananchi waendelee kuhimizwa kutunza chakula walichonacho kwani wakati mwingine kunapokuwa na mvua huwezi kuvuka kwenda sehemu nyingine na jukumu la kutunza chakula ni jukumu la familia.

Matangazo

  • MATOKEO DARASA LA SABA December 01, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2023. December 14, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2022 January 29, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023 June 11, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Wananchi Chinangali II Wapokea Neema Ya Mradi Wa Milioni 261

    May 06, 2025
  • "Fanyeni Kazi Kama Vikundi Pasipo Kutegeana" Mhe. Mayanja

    April 11, 2025
  • TSC Chamwino Yawapatia Tuzo Walimu Kwa Ufaulu Mitihani Ya Kitaifa

    March 27, 2025
  • Wakuu Wa Shule Wapatiwa Mafunzo Ya Mfumo Wa NeST

    March 21, 2025
  • Angalia Zote

Video

UTEKELEZAJI, UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA CHAMWINO
Video Zaidi

Viunganifu vya Haraka

  • Mafanikio ya Miaka Miwili ya Mhe. Rais
  • Mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2018
  • Historia ya Halmashauri
  • Dira na Dhima
  • Kituo cha Biashara
  • Kuonana na Mwenyekiti
  • Huduma za Watumishi
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganishi

  • Tanzania
  • PRo-RALG
  • Tovuti ya Wilaya ya Bahi
  • Parliament of Tanzania
  • Dodoma
  • Utumishi

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Counter Widgets

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    Sanduku la posta: 1126 Dodoma

    Simu ya Mezani: 026 296 1511

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.